MZOZO WA MAPENZI WAUA MKE SINGIDA, MWINGINE AJIUA BAADA YA KUMTIA
UJAUZITO BINAMU YAKE
![]() |
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela |
MKAZI
wa Kijiji cha Mwasutianga, Kata ya Irisya, wilayani Ikungi, Singida,
Mwanahamisi Mwangu (72), amekufa baada ya kupigwa mateke na ngumi na mumewe,
Salehe Mohammed (75) kutokana na ugomvi baina ya marehemu na mke mwenzie
wakigombea ndoo ya maji.
Tukio hilo
limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 7 mchana wakati wakiwa shambani wakipanda
mazao.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema siku ya tukio Mwanahamisi
alikuwa shambani na mumewe pamoja na mkewe mdogo, Fatuma Ramadhani (55).
Walikuwa wakipanda mtama, lakini ghafla ulizuka ugomvi wa kugombea ndoo
iliyokuwa na maji.Alisema katika ugomvi huo kila mmoja akidai ndoo hiyo ni mali yake, ndipo mume wao alipoamua kuingilia ugomvi huo.
“Mtuhumiwa mzee Salehe katika ugomvi huo alikuwa upande wa mke mdogo ndipo alianza kumpiga mateke na ngumi mkewe mkubwa Mwanahamisi na kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema Kamwela.
Alisema polisi wanamshikilia mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya upelelezi kukamilika.
Katika tukio jingine, Shauri Samwel (22) mkazi wa Kijiji cha Tyeme, wilayani Iramba, amefariki dunia baada ya kunywa vidonge vya kuhifadhia nafaka.
Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 31 mwaka jana, saa 12 jioni katika zahanati ya Kijiji cha Tyeme wakati Shauri akiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda Kamwela alisema chanzo cha kunywa vidogo hivyo ni hofu aliyokuwa nayo Shauri kutokana na kumtia ujauzito binamu yake.
No comments:
Post a Comment