AUA MKE NA MTOTO KUTOKANA NA ATHARI ZA DAWA YA
SARATANI
![]() |
Jean na mwanaye Sarah enzi za uhai wao |
Peter
Redfern alimnyonga mkewe kabla ya kumshambulia kwa shoka na kumuua mtoto wake
msichana Sarah katika mtaa wa Wath-upon-Dearne mwaka jana.
Redfern,
mwenye umri wa miaka 70, alihukumiwa kifungo cha miaka 17 baada ya jaji kusema
kuwa ni adhabu ya kutosha ambapo Redfern huenda akafa akiwa jela.
Miili
ya Bi Redfern na mwanawe Sarah, ilipatikana baada ya Redfern kupigia simu
polisi na kuwaambia kuwa amewaua mkewe na mwanawe.
Wawili
hao walipatikana wakiwa wafunikwa nyuso zao kwa karatasi za plastiki
Sheffield
anaugua aina ya Saratani ya mifupa ambayo haina tiba na ugonjwa wake
uligunduliwa Mei mwaka 2013 na alikuwa amekubali kushirikishwa kwenye utafiti
wa matibabu ya mchanganyiko wa dawa maalum kujaribu kumtibu.
Jaji
alimwambia kuwa dawa alizokuwa anatumia ziliweza kuathiri fahamu lakini sio kwa
kiasi kikubwa cha kumfanya kuwa muuaji.
Redfern
wakati wote alikuwa analia jaji alipomkumbusha matukio ya mauaji hayo. Hata
hivyo jaji alimwambia kuwa alifanya mauaji hayo akiwa mwingi wa fahamu kwani
aliyapanga mwenyewe.
"Wakati
Sarah alipowasili nyumbani, ulimkaribisha kwa karatasi ya plastiki na shoka
vyote ulivyotumia kumuua. Na ulipogundua kuwa mtoto wako alikuwa ameshuhudia
mauaji hayo, naye pia ukamuua ,'' alisema jaji
Hata
hivyo jaji alipokuwa anatoa hukumu, alizingatia ugonjwa wa mshitakiwa ndipo
akaamua kumfunga miaka 17 jela. Na pia alisema kuwa kama isingekuwa ugonjwa
wake pamoja na athari za dawa anazotumia, huenda asingefanya kitendo kama
hicho.
Redfern
alikiri kufanya mauaji hayo.
BBC
No comments:
Post a Comment