Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua
Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Uteuzi
huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha 13(i) cha
Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa Mwenyekiti na
Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013.
Aidha
Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema ,Dr. Vicensia
Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Bishop Hiluka kutoka
Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika kipindi cha
miaka mitatu ijayo.
Wajumbe
wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ntobi
Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo ambaye ni
Katibu wa Bodi ya Filamu.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI (MAELEZO)
No comments:
Post a Comment