MASHOGA KUUAWA KWA MAWE NCHINI
NIGERIA
Maafisa
wakuu Kaskazini mwa Nigeria, wanasema kuwa wamewafikisha katika mahakama ya
kiisilamu wanaume 11 wanaoshukiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kamishna
mkuu wa sheria za kiisilamu katika jimbo la Bauchi, alisema kuwa wanaume hao
walizuiliwa mwezi jana na ikiwa watapatikana na hatia huenda wakahukumiwa kifo
kwa kupigwa mawe.
Walisema
kuwa mmoja wa washukiwa ambaye ni mkristo, atashitakiwa katika mahakama
nyingine ya kiserikali.
Aidha
kamishna amekanusha madai kuwa wanaume hao waliteswa wakiwa wanazuiliwa.
Mapema
mwezi huu Rais Goodluck Jonathan alitia saini sheria inayotoa adhabu kali kwa
watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Afisaa
mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa mataifa, Navi Pillay aliikosoa sheria
hiyo kwa kusema imehatarisha zaidi maisha ya wapenzi ya jinsia moja nchini
Nigeria.
BBC
No comments:
Post a Comment