YALIYOJIRI TFF LEO
WACHEZAJI 30 WA TWIGA STARS WAITWA
KUIVAA ZAMBIA
KOCHA Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian
Kaijage ametaja kikosi cha wachezaji 30 wanaoingia kambini kesho (Januari 15
mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya Zambia mwezi ujao.
Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia itafanyika jijini Lusaka.
Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia itafanyika jijini Lusaka.
Donisia Daniel (Lord Baden Sekondari), Esther Chabruma (Sayari Queens), Evelyn Sekikubo (Kwimba Chuoni), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Issa (Evergreen) na Fatuma Mustapha (Sayari Queens).
Fatuma Omari (Sayari Queens), Happiness Hezron (Copa Coca-Cola Ilala), Maimuna Hamisi (U20 Tanzanite), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Real Tanzanite), Mwapewa Mtumwa (Sayari Queens), Najiat Abbas (Makongo Sekondari) na Neema Paul (U20 Tanzanite).
Pulkeria Charaji (Sayari Queens), Semeni Abeid (Real Tanzanite), Shelder Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari Queens), Theresa Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).
Katika hatua nyingine, TFF imepokea kwa masikitiko kifo cha mwanzilishi wa wa timu ya Oljoro JKT, Kanali Mmari kilichotokea jana (Januari 13 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kanali Mmari ambaye aliasisi timu hiyo na kuifikisha hadi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa baada ya kupata ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani, Januari Mosi mwaka huu.
TFF imesema msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani mbali kuasisi timu ya Oljoro JKT alikuwa mhamasishaji mkubwa wa mchezo huo mkoani Arusha, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF imetoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mmari, klabu ya Oljoro JKT, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (ARFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Wakati huo huo: TFF imeteua maofisa wanaoanza leo (Januari 14 mwaka huu) kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ukaguzi huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.
Viwanja vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza), Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage (Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora (Iringa).
Kumbukumbu ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani), Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui (Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), Umoja (Mtwara) na Vwawa (Mbozi).
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.

No comments:
Post a Comment