Friday, January 3, 2014

MWANAMKE AUAWA  NA MUMEWE BAADA YA  KUFUMANIWA AKIZINI NA BINAMU YAKE MBEYA

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi
Mwanamke mmoja mkazi wa Inyara jijini Mbeya, Huruma Laiton (20) ameuawa kwa kipigo kutoka kwa mumewe baada ya kumfumania akiwa anafanya mapenzi na binamu yake.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi, alisema  mwanamke huyo aliuawa juzi majira ya saa 11:00 jioni nyumbani kwake katika Kijiji cha Inyara.
Alisema tukio hilo la kinyama linadaiwa kufanywa na mume wa marehemu, Ezekiel Mwakabenga (21) ambaye anadaiwa kumpiga mkewe kwa kutumia ngumi, fimbo na mateke na kumsababishia majeraha makubwa ambapo alikimbizwa katika hospitali ya rufaa jijini humo na kufariki dunia akiwa anapata matibabu.
Msangi alisema Mwakabenga ambaye ni mfanyabiashara alimkuta mkewe akifanya mapenzi na binamu yake ndani ya nyumba yao, kitendo ambacho kilimchukiza, hivyo kuamua kumpiga.

Mwilii wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.

No comments: