Tuesday, December 24, 2013

SELESTIN MWESIGWA KATIBU MKUU TFF


TFF, Shirikisho la Soka Tanzania, leo limetoa Taarifa iliyosainiwa na Rais wake, Jamal Malinzi, ambayo imetangaza Maofisa wake Waajiriwa pamoja na Viongozi wa Kamati zake mbalimbali kama ilivyoamuliwa kwenye Kiakao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichokaa Tarehe 22-12-2013.
YAFUATAYO NI MAAMUZI YAO:
1.  1. KATIBU MKUU [GENERAL SECRETARY]
Katibu Mkuu wa TFF atakuwa ni Bwana Selestin Mwesigwa.
Bwana Mwesigwa amezaliwa Mwaka 1970. Ana Digrii ya masuala ya kimataifa toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ana Diploma ya Mafunzo ya Sheria.
Pia amefanya kozi kadhaa za utawala ndani na nje ya Nchi zikiwemo kozi za utawala wa mpira zilizotolewa na FIFA. Ajira yake ya mwisho alikuwa ni Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga.
Bwana Mwesiga anaingia TFF akiwa na uzoefu mkubwa wa masuala ya uongozi
1.  2. MKURUGENZI  WA VYAMA WANACHAMA NA MASUALA YA KISHERIA [DIRECTOR OF MEMBER ASSOCIATIONS AND LEGAL AFFAIRS]
Bwana Evodius Mtawala
1.  3. MKURUGENZI WA MASHINDANO [COMPETITIONS DIRECTOR]
Bwana Idd Mshangama atakaimu nafasi baada ya Waombaji kutofuzu na nafasi itatangazwa tena.
1.  4. Mkurugenzi wa ufundi [Technical Director]
Bwana Salum Madadi atakaimu baada Waombaji kutokidhi vigezo.
1.  5. MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA [DIRECTOR OF FINANCE AND ADMINISTRATION]
Bwana Danny Msangi kukaimu baada Waombaji kutokidhi vigezo.
1.  6. AFISA HABARI WA TFF [MEDIA OFFICER]
Ataendelea kuwa Bwana Boniface Wambura Mgoyo.
AJIRA ZITAANZA Januari 1.
UTEUZI WA KAMATI YA UCHAGUZI NA KAMATI YA RUFAA YA UCHAGUZI
-Kamati za Sheria: Uteuzi utafanywa baadae.
KAMATI YA UCHAGUZI [ELECTIONS COMMITTEE]
Advocate Melchesedeck Lutema-Mwenyekiti
Advocate Walter Chipeta-Makamu Mwenyekiti
Hamidu Mahmoud Omar-Mjumbe
Jeremiah John Wambura-Mjumbe
Hassan Dalali [Mjumbe]
KAMATI YA RUFAA YA UCHAGUZI [ELECTIONS APPEAL COMMITTEE]
Advocate Julius Lugaziya-Mwenyekiti
Advocate Mwita Waisaka-Makamu Mwenyekiti
Juma Abeid Khamis-Mjumbe
Rashid Dilunga-Mjumbe
Masoud Issangu-Mjumbe
BEACH SOCCER SUB COMMITTEE
KAMATI NDOGO YA KAMATI YA MASHINDANO INAYOHUSIKA NA MPIRA WA UFUKWENI
Ahmed Mgoyi-Mwenyekiti
Shafii Dauda-Makamu Mwenyekiti
Deo Lucas
Juma Mgunda
Boniface Pawasa
Joseph Kanakamfumu
John Mwansasu

No comments: