AMCHARANGA MAPANGA NA KUMKATA MKONO MCHUMBA WAKE KWA
WIVU WA KIMAPENZI
Huko
Wilayani Liwale Mkoani Lindi, Mkazi Mmoja wa kijiji cha Naluleo aliefahamika
kwa Jina la Shida Mapele amejeruhiwa vibaya kwa Mapanga na Mchumba wake na
kumsababishia ulemavu wa kudumu baada ya kumkata mkono wa kulia na kumjeruhi
katika baadhi ya viungo vyake kutokana na wivu wa kiampenzi.
Licha ya Mtuhumiwa kufikishwa mbele
ya Sheria,Wanawake wilayani Humo wametakiwa kutetea haki zao huku wakiomba sheria
ichukue mkondo wake dhidi ya ukatili huo uliofanywa na Bw. Ally Burian ambae
anashiliwa na Jeshi la Polisi.
Mratibu wa Asasi ya kutetea wanawake
na watoto(Liwopac)Bi Hidaya Chikawe alieleza kuwa licha ya harakati
zinazofanywa na wanawake kuelimisha jamii Bado Vitendo hivyo vinashika kasi
wilayani humo.
“Hakika kwa tukio hili ni Ishara tosha inayodhihirisha kuwepo kwa ukatili
wilayani humu,Hapo Awali tulizoea kusikia katika mikoa ya wenzetu lakini sasa
Dunia imebadilika tunashuhudia matukio haya mara kwa mara”alieleza
Chikawe.
Aidha aliwataka akina mama wa liwale
kuanza kujitetea kwa kufichua uhalifu unaojitokeza kutokana na Takwimu ya mwaka
jana inaonyesha matukio hayo kuwepo kwa 2% lakini sasa hali inaongezeka kila
mara hususan kipindi hiki cha mauzo ya korosho.
Kwa Upande wao baadhi ya akinamama
walisema licha ya historia ya matukio mabaya kutokea wilayani humo
wameguswa na tukio hilo huku wakitoa
wito kwa jamii na serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wanaobanika na
kukamatwa.
Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wamekuwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo hivi
karibu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi
wa Polisi Bi Renatha Mzinga alianzisha kampeni ya kutoa elimu kwa jamii
kuhusiana na matukio hayo katika maadhimisho ya siku 16 za ukatili dhidi ya
Mwanamke ambapo walifanikisha kutoa misaada na usafi katika kambi ya wazee na
walemavu.
No comments:
Post a Comment