ATUPWA
JELA MAISHA BAADA YA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA SITA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani
Nzega, Tabora, imemhukumu Juma Lufunga (26) kifungo cha maisha jela baada ya
kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi
Joseph Ngomelo alisema Lufunga (26) ametiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto
mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali na hivyo kustahili
kifungo cha maisha gerezani ili adhabu yake iwe fundisho kwa watu wengine wenye
tabia za aina hiyo.
Alisema vitendo vya ulawiti wa
watoto wadogo, vimekuwa vikiongezeka kila kukicha na kusababaisha jamii ishindwe
kufanya kazi zingine za maendeleo kwa hofu juu ya watoto wao kwa kuwa watu
wazima wamekuwa ni tatizo hasa wanaume.
Kabla ya hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo
Juma Lufunga akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliiomba mahakama impunguzie
adhabu kutokana na yeye kuwa ni mwathirika wa virusi vya Ukimwi, hata hivyo
mtuhumiwa huyo alipoombwa vyeti vya uthibitisho hakuweza kuwasilisha
mahakamani.
Awali, Mwendesha mashitaka wa Jeshi
la Polisi, Melito Ukongoji alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 24 mwaka 2012
majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Mwanihara, Lufunga alimlawiti mtoto wa
kaka yake na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.
Melito alidai taarifa ya daktari
ilithibitisha unyama aliofanyiwa mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.
No comments:
Post a Comment