Monday, December 16, 2013

UEFA CHAMPIONZ LIGI,DROO YAFANYIKA, ARSENAL USO KWA USO NA MABINGWA BAYERN
OLYMPIAKOS v MAN UNITED, GALATASARAY v CHELSEA
DROO ya Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, imefanyika leo
huko Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi, Bayern Munich wamepangiwa kucheza na Arsenal.
Mabingwa wa England, Manchester United, wao watacheza na Olympiakos ya Ugiriki na Chelsea itakutana na Galatasaray ya Uturuki.
DROO KAMILI:
Manchester City v Barcelona
Olympiakos v Manchester United
Arsenal v Bayern Munich
Zenit v Borussia Dortmund
Schalke v Real Madrid
Galatasaray v Chelsea
Bayer Leverkusen v PSG
Milan v Atlético Madrid

Mechi za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa hapo Tarehe 18 na 19 Februari na Marudiano ni Februari 25 na 26.

RAUNDI ya MTOANO ya TIMU 16
-MECHI ZA KWANZA: 18–19 & 25–26 Februari 2014
-MARUDIANO: 11–12 & 18–19 Machi 2014
ROBO FAINALI
-DROO: 21 Machi 2014
-MECHI ZA KWANZA: 1–2 Aprili 2014    
-MARUDIANO: 8–9 Aprili 2014
NUSU FAINALI
-DROO: 11 Aprili 2014
-MECHI ZA KWANZA: 22–23 Aprili 2014
-MARUDIANO: 29–30 Aprili 2014
FAINALI
4 Mei 2014 Estádio da Luz, Lisbon, Portugal

No comments: