YANGA MBENDEMBENDE YABANJULIWA 3- 1 NA SIMBA
NANI MTANI JEMBE TAIFA LEO
Kikosi cha simba |
Kikosi cha yanga |
Wekundu wa Msimbazi simba ya jijini Dar es
Salaam leo imefanikiwa kwa mara nyinge kuzima kidomo domo, mikogo na mbwe mbwe
za kila namna za watani wao wa jadi Yanga kwa kuwafunga magoli 3-1 katika
mchezo maalum wa NANI MTANI JEMBE mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam hii leo.
Katika mchezo huo Magoli ya simba yaliwekwa
kimiani na mshambuliaji wake mahiri mwenye kasi nyingi na mbinu lukuki za
ufungaji Hamisi Tambwe ambaye alipachika magoli 2 huku bao la tatu likifungwa
na mchezaji aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mtibwa Awazi Juma huku goli la
Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
No comments:
Post a Comment