Thursday, November 28, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE, MAN UNITED, REAL, PSG ZASONGA
Mabingwa wa England, Manchester United, Usiku huu wametinga kwa kishindo kikubwa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL baada ya kuitwanga Timu iliyo Nafasi ya Pili kwenye Bundesliga, Bayer Leverkusen, Bao 5-0 wakiwa Nyumbani kwao huko Germany.
Bao za Man United zilifungwa na Antonio Valencia, Dakika ya 22, Spahic, alijifunga mwenyewe Dakika ya 30, Jonny Evans, 65, Chris Smalling, 77, na Nani, Dakika ya 88.
Wakiwa hawafunguki kwao na Msimu huu wameshinda Mechi zote Uwanjani kwao kasoro Sare na Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, Bayer Leverkusen, walipewa nafasi kubwa lakini walijikuta wako hoi na sasa wamepitwa kwenye Msimamo wa Kundi hili na Shakhtar Donetsk ambayo leo imeitwanga Real Sociedad Bao 4-0.
Kwenye Mechi hii, Man United walivaa utepe Mweusi mkononi kuomboleza Kifo cha Lejendari Nahodha wao, Bill Foulkes, aliefariki Wiki hii akiwa na Miaka 81, ambae alichezea Klabu hiyo Mechi 688 ambazo zimepitwa tu na Sir Bobby Charlton, Ryan Giggs na Paul Scholes.

MATOKEO KAMILI:
Jumatano 27 Novemba 2013
Bayer 04 Leverkusen 0 Manchester United 5
FC Shakhtar Donetsk 4 Real Sociedad de Fútbol 0
Real Madrid 4 Galatasaray 1
Juventus 3 FC København 1
RSC Anderlecht 2 SL Benfica 3
Paris Saint-Germain 2 Olympiacos 1
PFC CSKA Moskva 1 FC Bayern München 3
Manchester City 4 FC Viktoria Plzeň 2

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
[Timu 8 Bado 8]
-Bayern Munich
-Manchester City
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Chelsea
-Manchester United
-PSG
-Real Madrid

No comments: