Wednesday, November 27, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE, CHELSEA YAFUNGWA LAKINI YASONGA, ASERNAL KIDEDEA LAKINI BADO, BARCELONA CHALI LAKINI YAFUZU

Chelsea wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, licha ya kufungwa Bao 1-0 na FC Basel hapo Jana huko Uswisi kwenye Mechi ya Kundi E.
Barcelona, wakicheza bila ya Nyota wao Lionel Messi na ambao kabla ya Mechi yao ya Jana walikuwa wameshatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, walifungwa Bao 2-1 na Ajax huko Amsterdam na hicho ni kipigo cha kwa kwanza kwao Msimu huu chini ya Meneja wao mpya Gerardo Martino.
Ajax sasa watasafiri kwenda Italy Mwezi ujao kucheza na AC Milan ambao Jana waliitandika Celtic 3-0 huko Scotland na Matokeo ya Mechi hii kuamua nani ataungana na Barca.
Katika Kundi F, Timu 3, Arsenal, Napoli na Borussia Dortmund, zina uwezo wa kupata Nafasi mbili za kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada Arsenal kuifunga Olympique Marseille 2-0 na Borussia Dortmund kuichapa Napoli 3-1.
Arsenal watamaliza Ugenini na Napoli na Dortmund pia wako Ugenini kucheza na Marseille ambayo imeshaaga Mashindano.
Mechi za Jana za Kundi G zote zilimalizika kwa Sare ya 1-1 wakati lakini moja kati ya Zenit St Petersburg na Porto bado zina nafasi ya kuungana na Atletico Madrid Raundi ijayo.

MATOKEO:
Jumanne 26 Novemba 2013
FC Steaua Bucureşti 0 FC Schalke 0
FC Basel 1 Chelsea 0
Arsenal 2 Olympique de Marseille 0
Borussia Dortmund 3 SSC Napoli 1
FC Porto 1 FK Austria Wien 1
Football Club Zenit 1 Club Atlético de Madrid 1
Celtic FC 0 AC Milan 3
AFC Ajax 2 FC Barcelona 1

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
[Timu 5 Bado 11]
-Bayern Munich
-Manchester City
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Chelsea

RATIBA YA LEO
Jumatano 27 Novemba 2013
Bayer 04 Leverkusen v Manchester United FC
FC Shakhtar Donetsk v Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid CF v Galatasaray A.Ş.
Juventus v FC København
RSC Anderlecht v SL Benfica
Paris Saint-Germain v Olympiacos FC
PFC CSKA Moskva v FC Bayern München [20:00]
Manchester City FC v FC Viktoria Plzeň

No comments: