MAUAJI TENA, AMUUA
MKEWE MJAMZITO KWA KUMPIGA MAWE, MATOFALI
![]() |
Marehemu Enea Kagi |
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
linamshikilia Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini Dar es
Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na
matofali hadi kumuua.
Philemon
anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili
kabla ya kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita nyumbani kwake
Wazo-Hill.
Akisimulia
mkasa huo jirani wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid
alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.
“Nilitoka
nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini nilihofia maisha yangu hivyo
ilinibidi niwaite vijana wa ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo
la tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani kama mtu
aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa ameshamuua mkewe.
“Baada ya
kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani na kwenda kujificha uvunguni
kwenye kitanda huku watoto wao watatu wakiwa wamelala.
“Bila
kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata na kuwasiliana na Askari wa
Kituo cha Polisi cha Wazo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni
mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za
kipolisi,” alisema Fikiri.
Kufuatia
tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika katika Hospitali ya
Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa
akiwa amefia tumboni.
Miili hiyo
ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka huu katika kaburi moja kwenye
Makaburi ya Madale, Dar es Salaam
GPL
No comments:
Post a Comment