AARON RAMSEY AWALIZA WAJERUMANI PALE ARSENAL ILIPOIKANDAMIZA BORUSSIA DORTMUND 1-0
ETO'O NAYE APELEKA KILIO KWA WAJERUMANI
WENGINE APIGA MBILI CHELSEA IKIUA SCHALKE 04.
MESSI NAYE , AIPIGIA MBILI
BARCA NA KUINYONGA AC MILAN ULAYA
BAO pekee
la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya
wenyeji Borussia Dortmund nchini Ujerumani.
Hilo
linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika michuano
ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza vyema usiku wa kuamkia leo kabla ya Arsenal kupata bao
lake, hawakuweza kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga.
Borussia
ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa, iliingia kwenye
mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart katika ligi
ya kwao, Bundesliga, lakini ilikalishwa na mtutu mmoja wa bunduki.
Katika mechi nyingine, Barcelona imeifunga AC Milan
mabao 3-1 Uwanja wa Camp Nou, Lionel Messi akifunga mawili dakika ya 30 na 83,
wakati lingine limefungwa na Busquets dakika ya 40, huku Pique akijifunga dakika
ya 45 kuwapatia wageni bao la kufutia machozi.
Nayo Chelsea imeifumua 3-0 Schalke 04, mabao ya
Samuel Eto'o dakika ya 31 na 54 na Demba Ba dakika ya 83.
Matokeo mengine
Ajax
|
Celtic
|
Basel
|
Steaua
Bucuresti
|
SSC
Napoli
|
Marseille
|
Zenit
Petersburg
|
FC
Porto
|
Atletico
Madrid
|
Austria
Wien
|
||||

No comments:
Post a Comment