HAYA SASA MAKUBWA, ASKOFU ADAIWA TALAKA NA MKEWE
|
| Dk Jacob Erasto Chimeledya kiongozi Anglikana Tanzania |
Askofu wa kanisa la
Anglikana Doyosisi ya Rorya John Adiema,amefunguliwa mashitaka ya madai
na mke wake wa ndoa ambapo pamoja na mambo mengine mwanake huyo ameimbiama hakama
ya hakimu mkazi mkoa wa Mara kutengua ndoa yao na kupewa talaka.
Kesi hiyo namba moja ya
mwaka huu ambayo inatajwa kuwa ya kwanza kutokea kwa kanisa hilo
nchini,ikihusu askofu kufikishwa mahakamani imepangwa kusikilizwa
Novemba 18 mwaka huu
katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mara mjini Musoma.
Mke wa kiongozi wa
mkuu wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya
Rorya Bi Peres
Adiema,akizungumza baada ya kufungua shauri hilo mahakamani hapo,amesema pamoja
na talaka pia anamdai mume wake huyo haki zake zote za msingi walizochuma
wakiwa kama wana ndoa.
Lukwangule blog

No comments:
Post a Comment