KENYA IMO MBIONI KUANZISHA SERA YA MKE MMOJA WATOTO WAWILI
Utafiti
uliofanywa nchini Kenya umeonesha taifa hilo litashindwa kufikia dira yake ya
maendeleo ya mwaka 2030 kutokana na wingi wa watu na sasa linataka kuanzishwa
sera ya mwanamke kutozaa zaidi ya watoto wawili.
Maeneo kame ya kaskazini mwa nchi hiyo, licha ya kuwa kwake na shida kubwa zaidi ya maisha, yametajwa na ripoti hiyo kuwa yanayoongoza kwa idadi kubwa ya vizazi.
Ingawa ripoti hiyo haisemi moja kwa moja, lakini inaelekea sana kupendekeza sera ya kila mwanamke kuzaa watoto wawili nchini Kenya kuwa jambo la lazima.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema kwamba hata kama sera hiyo itaanzishwa, italazimika kutanguliwa na mfumo mzuri sana wa kuisaidia, zikiwemo njia za kuimarisha uzazi salama, afya ya kimama na watoto wanaozaliwa na pia kampeni itakayokwenda hadi vijijini.
Kubwa zaidi ni kuhakikisha kuwa wasichana wengi zaidi kadiri inavyoyumkinika wanapatiwa elimu angalau mpaka ya sekondari, kwani utafiti huo ulionesha kwamba wanawake wenye watoto kidogo zaidi ni wale ambao angalau wamefikia kiwango hicho cha elimu.
Wakosoaji wa pendekezo hili la kuanzishwa kwa sera ya watoto wawili kwa kila mwanamke, wanasema kwamba hakuna uwiano kati ya idadi ndogo ya watu na kufikiwa kwa Dira 2030 inayoielekeza Kenya kuwa taifa lenye uchumi wa kati.
DW
No comments:
Post a Comment