BLATTER ASEMA MOROCCO WAPO TAYARI KWA KLABU BINGWA
ZIKIWA zimebaki wiki mbili kabla ya kuanza kutimua
vumbi kwa michuano ya Klabu ya Bingwa, rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA
Sepp Blatter anaamini kuwa wenyeji Morocco wako tayari kwa ajili ya michuano
hiyo. Blatter amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuelezea hatua za mwisho za maandalizi ya michuano hiyo pamoja na timu
zitakazoshiriki. Rais huyo amesema timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni
pamoja na Guangzhou Evergrade ya China ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa
barani Asia, Bayern Munich mabingwa wa Ulaya na Al Ahly mabingwa wa
Afrika. Wengine ni Auckland City mabingwa Oceania, Monterrey mabingwa wa
CONCACAF, Atletico Mineiro mabingwa wa Amerika Kusini na Raja Casablanca ambao
wameingia katika michuano hiyo kama wenyeji.
No comments:
Post a Comment