BUKINABE WAENDA FIFA KUPELEKA MALALAMIKO JUU YA REFA DIATTA
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA, limethibitisha kupata
malalamiko kutoka Shirikisho la Soka la Burkina Faso kuhusiana na mchezo wao wa
kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ambapo nchi hiyo ilifungwa bao 1-0 na
Algeria. Maofisa hao wa Burkinabe wameiandikia FIFA kulalamikia baadhi ya
maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi Badara Diatta wa Senegal wakati wa mchezo huo,
maamuzi ambayo yalipelekea kukataliwa kwa bao lao katika kipindi cha
kwanza. Shirikisho hilo pia limelalamikia kadi ya njano aliyopewa nahodha
wa Algeria Madgid Bougherra wakidai kuwa alistahili kadi nyekundu baada ya
kumfanyia madhambi nahodha wa Burkinabe Charles Kabore katika eneo la
hatari. Uamuzi wa FIFA unatarajiwa kuhusiana na tukio la mchezo huo
unatarajiwa kutolewa Desemba 5, siku moja kabla ya ratiba kamili ya Kombe la
Dunia.

No comments:
Post a Comment