MKE AKATWA MGUU KWA PANGA NA MUMEWE KWA WIVU WA KIMAPENZI HUKO TARIME
![]() |
Bi Ghati Chacha |
Mwanamke
mmoja Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha
Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia
na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.
Akisimulua
mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza
vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya
Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.
“Aliniuliza kwa
nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba
kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa
kidole” alisema Ghati.
Wakati
anamwonesha lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata
alifikiri kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda sehemu kwa
kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia
mji kama uko sawa alafu arudi kulala.
Alipoipata ile
panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile
akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa
kulia ukakatika kama unavyoona” alieleza kwa masikitiko akiifunua
kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya
Tarime.
Wakati
anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika
kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama
hivyo kusikika katika maeneo hayo.
“Baadaye walikuja
na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia
baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza
katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa” alieleza .
Hata
hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za
mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
“
Nimeishi
naye kwa miaka minne sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri,
tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka lingine ni baada ya kuoa
mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu”
alisema Ghati.
Ghati
hataweza kurudiana na mume wake huyo kwa kitendo alichomfanyia kwa vile
amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jera ili
ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.
” Naomba
serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina
uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na
mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula” alisema.
Wananchi
walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa na kukilaa kuwa
kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .
“
Sikifurahii
kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako
na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku kutuona
sisi ni wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa,
mahakama imuhukumu huyu mtu adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho
kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.
Jeshi
la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia
kipande cha mguu na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.
Hata
hivyo siku moja baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa
kusaidiana na nguvu za wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya
Tarime kujibu mashitaka hayo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime
(ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwita alikiri
kumsababishia mke wake kilema wa maisha.
“ Vitendo vya
kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo
lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote”
alisema Kamugisha kwa nija ya simu
No comments:
Post a Comment