ZAMBIA IMETOA VIBALI VYA KUKAMATWA KWA
WACHEZAJI WAKE WATATU KWA KUKOSA MECHI ZA KIRAFIKI
Zambia imetoa vibali vya kukamatwa kwa wachezaji wake watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mjini Beijing China. Hata hivyo Zambia ilishindwa na Brazil mabao mawili kwa nunge. Klabu ya DRC TP Mazembe ilisisitiza kuwa wachezaji hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala walijeruhiwa na kusababisha mgogoro kati ya shirikisho la soka la Zambia na serikali ya Zambia. Baada ya wachezaji hao kufanyiwa ukaguzi mjini Lusaka, shirikisho la soka la Zambia likasisitiza kuwa bado wanaweza kusafiri kwenda China kwa mchuano huo,lakini klabu ya Mazembe ambako wachezaji hao hucheza soka ya kulipwa ikawataka kurejea.
Hatua
hiyo ilisababisha serikali ya Zambia kuingilia kati kwa kuwapokonya wachezaji
hao pasi zao za usafiri ili kuwazuia kwenda kuchezea klabu yao mjini
Lubumbashi.
Hata
hivyo, wachezaji walifanikiwa kuvuka mpaka na wanaaminika kuwa nchini DR Congo.
Shirikisho
la soka la Zambia limeandikia barua shirikisho la soka duniani Fifa, na
kulalamika kuwa klabu ya Mazembe haikuwaruhusu wachezaji hao kushirki majukumu
yao ya kimataifa.
Zambia
ilishindwa kwenye mechi hiyo ya kimataifa mjini Beijing
Zambia
ambao ni mabingwa wa kombe la taifa bingwa Afrika walikuwa wanashirki mechi yao
ya kwanza wakiongozwa na kocha wao mpya Patrice Beaumelle, ambaye alichukua
usukani siku nane zilizopita baada ya Herve Renard kucha kazi.
BBC
No comments:
Post a Comment