FIFA YAANZISHA MTANDAO WA UHAMISHO NDANI YA NCHI (DTMS), GHANA YAITAKA FIFA KUONDOA MECHI NCHINI MISRI
LEO
FIFA inazindua Mtandao wa Domestic Transfer Matching System (DTMS) ili
kuzisaidia Mchi Wanachama wake kuendesha Uhamisho wa Wachezaji ndani ya Nchi
zao.
DTMS
unachukua muundo wa ITMS (International Transfer Matching System) ambao umekuwa
ukimudu Uhamisho wa Kimataifa wa Wachezaji na hii DTMS itagawiwa kwa Nchi
Wanachama zaidi ya 200 na Klabu 6,500.
DTMS
na ITMS zinaingiliana na zinapatika katika sehemu moja ya Mtandao.
FIFA
imesema DTMS itazidisha udhiti wa Uhamisho wa Wachezaji kwa kuwepo uwazi wa
kuzingatia Kanuni za Uhamisho.
Pia
Mtandao huo utarahisisha Malipo ya Uhamisho na kuondoa utata uliokuwepo hivi
sasa wa Klabu kurushana Fedha katika Uhamisho.
FIFA
imesema moja ya faida kubwa ya kutumia DTMS ni kufanya Uhamisho wa Wachezaji
uwe mwepesi na wa haraka kukamilisha huku kumbukumbu zake zikiwa rahisi
kuhifadhiwa.
DTMS
inatarajiwa kuanza rasmi kutumika na Nchi Wanachama wa FIFA Mwakani.
GHANA YAITAKA FIFA KUIONDOA MECHI
NCHINI EGYPT
GHANA
wameitaka FIFA kuitazama upya Mechi yao na Egypt ya kuwania kwenda Brazil
kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwakani iliyopangwa kuchezwa Mjini Cairo hapo
Novemba 19 ili ihamishwe toka Nchini Egypt kwa vile hali ya usalama inatisha.
Chama
cha Soka cha Ghana, GFA, kimeiandikia FIFA kuitaka kutazama hali ya usalama
Nchini humo na kuangalia upya Mechi hiyo kuchezwa Mjini Cairo.
Ghana
imeitaka FIFA kutazama uamuzi wa Misri kuiweka Mechi hiyo Mjini Cairo na
kuchezwa mbele ya Watazamaji kitu ambacho hakijafanyika Nchini humo kwa Miaka
miwili ambapo Watazamaji wamekuwa hawaruhusiwi kuingia kwenye Mechi kwa sababu
za kusalama.
Egypt
ilizuia Watazamaji kuingia kwenye Mechi baada ya Vifo vya Watu 74 kwenye Uwanja
Mjini Port Said lakini kwa Mechi za Timu ya Taifa, Watazamaji wachache wamekuwa
wakiruhusiwa.
Kwa
sasa huko Egypt Mechi zote zimesimama isipokuwa zile za Timu ya Taifa na Klabu
mbili tu, Al Ahli na Zamalek, zilipokuwa zikicheza michuano ya CAF CHAMPIONZ
LIGI na Mechi zote hizo zimekuwa zikichezwa Mji mdogo wa El Gouna uliopo kando
kando ya Red Sea na bila ya Watazamaji kuwepo.
Lakini
kwa Mechi hiyo ya Ghana na Egypt hapo Novemba 19, ambayo itakuwa ni ya
Marudiano baada ya kucheza huko Kumasi, Ghana hapo Oktoba 15, imeamuliwa
kuchezwa Mjini Cairo mbele ya Mashabiki wao ili kuipa nafasi Egypt iweze kucheza
Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu Mwaka 1990.
No comments:
Post a Comment