MASHABIKI WA KIUME WAFUNGIWA KUANGALIA MECHI ZA BESIKTASI
KLABU ya
Besiktas ya Uturuki italazimika kucheza mechi nne za nyumbani bila ya mashabiki
wanaume baada ya rufani yao kutupiliwa mbali na Kamati ya Usuluhishi nchini
humo. Mechi kati ya Besiktas na timu za Rizespor, Kardermir Karabukspor,
Torku Konyaspor na Sivasspor zitahudhuriwa na mashabiki wanawake na watoto
pekee kufuatiwa wanaume kuzuiwa kutokana na vurugu mwishoni mwa mechi dhidi ya
Galatasaray mwezi uliopita. Mechi baina ya timu hizo ilivunja rekodi ya
mahudhurio na kufikia 76,712 lakini iliingia dosari kwa wachezaji kukimbia
katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo kujificha baada ya mamia ya mashabiki
kuvamia uwanja mwishoni mwa mchezo. Kocha wa Besiktas alipewa adhabu ya
kufungiwa mechi tatu na Shitikisho la Soka la nchi hiyo kufuatia kumshambulia mwamuzi
wakati klabu hiyo ilitozwa faini ya euro 21,000 kwa kushindwa kuwadhibiti
mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment