DROO YA AFCON KUFANYIKA JANUARI 31 AFRIKA YA KUSINI
DROO
ya kupanga Mechi za Mchujo za kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
Mwaka 2015, AFCON 2015, itafanyika huko Afrika Kusini hapo Januari 31.
CAF
imethibitisha kufanyika kwa Droo hiyo huko Mjini Cape Town wakati michuano ya CHAN ikiendelea humo
Nchini Afrika Kusini katika Miji ya Bloemfontein, Cape Town na Polokwane.
Fainali
za AFCON 2015 zitafanyika huko Nchini Morocco na Mechi za kusaka Timu
zitakazotinga Fainali zitachezwa katika Kipindi kifupi cha Miezi mitano tu kati
ya Julai na Novemba Mwakani.
Mfumo
wa kupata Timu zitakazoingia Fainali ni kuchezwa Raundi ya Awali kati ya Julai
na Agosti, itakayochezwa kwa mtindo wa Nyumbani na Ugenini, na kufuatia hatua
ya Makundi itakayochezwa kuanzia Septemba.
Mechi
za Makundi zinatakiwa zichezwe ndani ya Wiki 6 kati ya Septemba na Novemba
kwenye Siku za Kalenda ya FIFA ya Mechi za Kimataifa na hivyo Mechi kuchezwa
mfululizo Ijumaa na Jumanne inayofuatia kama vile Ulaya wamekuwa wakifanya hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment