Friday, October 25, 2013

HATARI DANGURO LA WANAFUNZI LAGUNDULIKA JIJINI DAR

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam chini kamanda Suleiman Kova kwa kushirikiana na Global Publishers wamefanikiwa kulifumua danguro linalodaiwa kufuga wanafunzi wa vyuo mbalimbali jijini Dar.
Wanafunzi  hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro hilo lililopo ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.
Awali kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, waandishi wa habari hizi waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia shilingi elfu mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na kuendelea.
 “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.” Akielezea shuhuda wa tukio hilo.
Baada ya kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo, Bila kusita, kamanda huyo aliteua vijana wake kutoka Kituo Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.

Wakati watuhumiwa hao wakishughulikiwa na polisi, mmoja wa wanafunzi hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.

Katika utetezi wake, mwanafunzi  huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.

Mwanafunzi mwingine aliyekamatwa katika tukio hilo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa mtu  mmoja aliyekuwa akiuza kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.

Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa wengi walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza mwili.

Baada ya kuhojiwa kuhusika na biashara haramu ya ngono na kukiri, watuhumiwa hao wote waliwekwa kituoni kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la kesi namba BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa wanafunzi  hao na wengine wengi jijini Dar, wamekuwa wakiaga kwao kuwa wanakwenda masomoni lakini kumbe wanaishia kwenye madanguro yaliyojazana jijini kwa ajili ya kujiuza.
Huku wazazi wakitoa fedha nyingi na huduma nyingine wakiamini watoto wao wanasoma, hali ni tofauti kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakiishia kwenye vitendo vya kihuni na kufeli masomo na maisha kwa jumla kisha kugeuka mzigo kwa familia.
Gazeti hili linawataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao wanaowasomesha ili kuwakanya juu ya kujiingiza kwenye uhuni ambao huhatarisha maisha yao -Mhariri.

GPL

No comments: