NYOTA WA ZAMANI WA BLACK STARS YA GHANA AFARIKI DUNIA
NAHODHA wa
zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Emmanuel Quarshie amefariki dunia baada ya
kuugua saratani ya koo kwa kipindi kirefu. Nahodha huyo alijulikana zaidi
wakati alikiongoza kikosi cha Ghana maarufu kama Black Stars kushinda taji la
Mataifa ya Afrika mwaka 1982. Miaka miwili baadae Quarshie aliendelea
kung’ara zaidi wakati akicheza katika klabu ya Zamalek ya Misri kwa kuiwezesha
klabu hiyo kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa barani
Afrika. Nguli huyo aliondoka Ghana Julai mwaka jana kwenda Misri kupatiwa
matibabu ambapo klabu yake ya zamani ya Zamalek ilidhamini matibabu yake.
No comments:
Post a Comment