MWALIMU ALIYEMBAKA MWANAFUNZI AENDA GEREZANI MIAKA 30
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na
kuchapwa viboko 30 mwalimu wa Shule ya Msingi Ingwachanya.
Mwalimu
huyo, Bw. Romanus Msango, mkazi wa Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani
kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) na kumuumiza
vibaya sehemu za siri.
Akisoma
hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Ludewa, Bw. Fredrick Lukuna, alisema mahakama imeridhika na ushahidi
uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuwa na shaka yoyote.
Alisema
mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(1) na 31(1) cha
kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine.
"Natoa
adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii kwani vinaleta madhara
makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya
kuambukiza," alisema.
Awali
ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Edison Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili
huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika Kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali.
Alisema
kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na
kumlawiti jambo ambalo lilimsababishia maumivu makali.
"Serikali
ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la
kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya
kazi yake, kuidharirisha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe
fundisho kwa walimu wengine," alisema.
Bw.
Kasekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu
alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao
walikimbia kwenda kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao
na kumpeleka kichakani.
Wak ati huo huo, watu wawili Bahati Mtega na Flowin
Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na
kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia
maumivu makali.
Majira.
No comments:
Post a Comment