LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO
LIGI ya Mabingwa barani Ulaya inaanza kutimua vumbi
rasmi leo kwa timu mbalimbali barani humo kuonyeshana kazi katika mechi za
hatua ya makundi.
Kwa upande wa kundi A tutashuhudia Manchester United
wakifungua dimba kwa kuikaribisha Bayer Liverkusen ya Ujerumani katika uwanja
wa Old Traford huku Real Sociedad ya Hispania wakipepetana na Shaktar Donetski
ya Ukraine. Mabingwa mara tisa wa michuano hiyo Real Madrid watakuwa
wageni wa Galatasaray ya Uturuki huku FC Copenhagen wakiwakaribisha mabingwa wa
soka wa Italia Juventus kwa mechi za kundi B.
Mechi za kundi C
itazikutanisha matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain ambao watakuwa
wageni wa Olympiacos ya Ugiriki huku Benfica ya Ureno ikiwakaribisha Anderlecht
ya Ubelgiji. Michezo mingine ya siku ya leo itakuwa ni pamoja na mabingwa
watetezi wa michuano hiyo Bayern Munich ya Ujerumani watakaikaribisha CSKA
Moscow ya Urusi huku Viktoria Plzen ya Jamhuri ya Czech wakiwakaribisha
matajiri wa Uingereza Manchester City katika mechi za kundi D. Mechi zote
zitachezwa katika muda mmoja wa saa nne kasorobo usiku za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment