Wednesday, September 18, 2013

MFALME MSWATI KUOA MKE WA 14
Msemaji wa ikulu ya Swaziland amesema Mfalme  Mswati III amemteua mwanamke wa umri wa miaka 18 anayeshindania tuzo ya urembo kumuoa awe mke wa 14
"Ninaweza kuthibitisha kwamba mfalme ameletea taifa  liphovela mpya (liphovela ni mchumba wa kifalme),” gavana wa ikulu ya Ludzidzini Timothy Mtetwa alisema.
Mswati, mwenye umri wa miaka 45 ndiye mfalme wa pekee aliyesalia mwenye mamlaka makuu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Kwa mujibu wa Mtetwa, Mfalme Mswati III alimtambulisha mwanamke huyo kwa jina Sindiswa Dlamini wakati wa Densi ya Tete.
Alikuwa amevalia manyoya mekundi kichwani – ishara ya ufalme.
Mwanamke huyo alimaliza shule ya upili ya St. Francis High School mjini Mbabane mwaka uliopita na akafika fainali ya shindano la urembo la Miss Cultural Heritage. Mshindi atatangazwa Septemba 28.
Harusi itafanyika tu ikiwa mchumba huyo atashika mimba. Dlamini wakati huo atakuwa mke wa 14 wa Mswati.
Wake watatu wametoroka nyumba ya mfalme huyo miaka ya hivi karibuni.
Wa majuzi zaidi, Malkia LaGija, alitoroka ikulu 2012 akidai kwamba alikuwa akichapwa na kuteswa kiakili.
Mwingine, LaDube, anadaiwa kupigwa baada ya kupatikana akishiriki ngono na waziri wa haki, ambaye ni rafiki wa karibu wa mfalme huyo.
Mswati alimteka nyara na kumuoa mfalme huyo akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2005.

No comments: