REFA ACHAPWA NA KUJISAIDIA HAPOHAPO KATIKA LIGI YA UJIRANI MWEMA HUKO SUMBAWANGA
Na Ernest Simya, Sumbawanga
Mwamuzi
na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya wilayani Sumbawanga mkoani
Rukwa wamelazwa kwenye kituo cha Afya cha Laela baada kushambuliwa na kwa
kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao katika mchezo wa Ligi ya ujirani mwema.
Katika
mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Kisalala kata ya Laela
Mwamuzi wa mchezo huo Eliaza Simsokwe ilipofika dk ya 75 alishambuliwa na
kundi la mashabiki na kumvua nguo zake wakiendelea kumpa kipigo
Kipigo
hicho kilisababisha mwamuzi huyo kujisaidia haja kubwa kipigo kinachodaiwa
kutolewa na wapenzi wa timu ya Serengeti FC wakipinga bao lililofungwa na
mchezaji wa timu pinzani ya Muchiza FC, Siyaye Mgonde wakidai alikuwa ameotea
kabla ya kufunga.
Meneja
wa Timu ya Serengeti FC ya Kisalala , Andrew William alisema kuwa baada ya
mwamuzi huyo kuvuliwa nguo na kupata kipigo hicho ilibidi baadhi ya wananchi
kuingilia kati na kumwokoa hatimaye mwanamke mmoja alimsaidia kwa kumfunga
khanga ya kumsitili kabla ya
kukimbizwa kituo cha Afya cha Laela kwa ajili ya matibabu.
Katika
vurugu hizo pia wachezaji wawili na kocha watimu ya Serengeti walijeruhiwa na
kulazwa kwenye kituo hicho cha Afya pamoja na uharibifu mkubwa wa pikipiki na
baiskeli 10 zilizokuwapo uwanjani hapo
Aidha
ugomvi huo uliibuka tena majira ya usiku nje ya uwanja ambako watu wanaodaiwa
kuwa ni wakazi wa kijiji cha Kisalala walivamia tena wachezaji wa timu ya
Serengeti FC na kumjeruhi Peter Willy alijeruhiwa kwa kupigwa panga kichwani na
kusababishiwa jeraha kubwa.
Kufuatia
hali hiyo uongozi wa Chama cha soka wilayani Sumbawanga (SURUFA) kupitia kwa
katibu wake, Kanyiki Nsokolo kimewatahadharisha washabiki wa mchezo huo
kuachana na vitendo vya vurugu kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwashambulia waamuzi wa mchezo kwa kuwapiga pale wanapochezesha michezo
mbalimbali.
Alisema
kufanyika kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kuendesha masuala ya soka kienyeji
pasipo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja mashindano hayo kufanywa pasipo kukishirikisha
chama cha soka cha wilaya sanjari na kutokuwapo kwa makocha na waamuzi
wenye sifa kwa ajili ya kuchezesha michezo mbalimbali ya soka.
No comments:
Post a Comment