Wednesday, August 14, 2013

MY BROTHER GRACIMO BAMBAZA MUNGU AMEMPENDA ZAIDI
Marehemu Gracimo Bambaza
Nikiwa na Marehemu Gracimo Bambaza siku ya send off yangu
ALIYEKUWA mfanyakazi wa kampuni ya Pride Media Ltd, kupitia kituo chake cha Pride Fm Radio tawi la Dar es salaam, Gresmo Bambaza, amefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo katika hospitali ya Ocean Road alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya koo.
Taarifa kutoka katika familia ya marehemu zinaeleza kuwa mipango ya mazishi inafanyika ili kuweza kusafirishwa kwa mwili wa marehemu kwenda kijijini kwao Wilayani Karagwe, Mkoani Kagera kwa mazishi.
Marehemu Gresmo Bambaza alizaliwa mwaka 1973, huko Karagwe mkoani Kagera, alipata elimu yake ya msingi mkoani Kagera, na elimu ya sekondari katika mkoa wa Mwanza.
Aidha alipata mafunzo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji ngazi ya cheti na Diploma katika chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) cha jijini Dar es salaam, na kuajiriwa katika kituo cha Habari cha Pride Fm Radio mwaka 2008, ambapo marehemu ameacha mjane na watoto wawili wa kike na kiume.
Nitamkumbuka gracimo kwa mengi kwani alikuwa mtu wangu wa karibu sana si katika maswala ya kazi tu, bali hata maswala binafasi, kwani yeye ndiye aliyekuwa mpambe wangu siku ya send off ikiwa ni maandalizi ya harusi yangu miaka miwili iliyopita.

Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu Gresmo Bambaza mahala anapostaili Amina.

No comments: