Thursday, August 15, 2013

ALIYEMZINI NG'OMBE ATUPWA JELA MIAKA 14 HUKO NCHINI KENYA
Bwana Jackson Kiruga
MWANAMUME mmoja aliyepatikana na hatia ya kumzini ng’ombe aina ya Freshian maeneo ya Nyeri amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela na mahakama.
Jackson Kiruga, 35, alihukumiwa katika mahakama Mukurwe-ini jana Jumatano.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu mwandamizi Wendy Kagendo alifadhaika kwamba maadili ya jamii yamedidimia huku visa vya watu kufanya ngono na wanyama vikiongezeeka kila uchao. Alisema kutokana na hayo hukumu kali ilifaa kutolewa ili kuzuia wengine kufanya vitendo hivyo.
Katika kesi hiyo, Jackson Kiruga alikuwa ameshtakiwa kwa kuvamia na kufanya mapenzi na ng’ombe wa Wanjiru Nyaga Julai 24 mwaka huu, katika kijiji cha Mihuti kata ndogo ya Gathia, Mukurwe-ini.
Katika ushahidi wake, Bi Wanjiru alisimulia mahakama alivyomfumania mwanamume huiyo aliyemtambua kama jirani yake akijamiiana na ng’ombe wake.
Bi Wanjiru alikuwa ameamka mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ili kumkama ng’ombe wake na kwa sababu kulikuwa bado na giza, alielekea kwenye zizi akiwa na tochi ili aweze kumpeleka ng’ombe wake mahali pa kukamiwa.
Bw Kiruga alikuwa amezama katika kitendo hicho hivi kwamba hakung’amua kufika kwa Bi Wanjiru kwenye zizi hadi pale alipopiga yowe.
Bi Wanjiru alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Mihuti na baadaye akamwarifu kiongozi wa eneo hilo, Bi Lucy Waringa, ambaye aliandamana naye hadi eneo la tukio. Baada ya kuthibitisha, kiongozi huyo aliandamana na wazee kadhaa hadi kwa mshukiwa na kumkuta bado analala na ndipo wakamtia mbaroni huku wakifanikiwa kupata suruali yake iliyokuwa na kinyesi na manyoya ya ng’ombe.
Bw Kiruga aliyeshtakiwa Julai 25 na akakanusha mashtaka hayo aliishangaza mahakama siku ya kusikilizwa kwa kesi yake baada ya kukubali mashtaka.
Hata hivyo, korti ilimshauri kuruhusu kusikizwa kwa kesi kwani kesi hiyo ilibeba hukumu kali.
Akijitetea, Kiruga aliiambia mahakama kwamba alikuwa ameingia kwake usiku uliopita akiwa amelewa chakari na kuacha mlango wazi na labda mtu alichukua suruali yake na kuipaka kinyesi cha ng’ombe.
Hata hivyo, akisoma hukumu yake, hakimu Wendy alitupilia mbali uwezekano wa jambo hilo kutokea huku akisema kwamba mshtakiwa hakuwa amedokeza nani angekuwa amefanya hivyo wala hakuwa ameonyesha kwa vyovyote vile kwamba Bi Wanjiru angekuwa na nia ya kumsingizia kesi hiyo.
Vilevile, hakimu Wendy alisemaBw Kiruga hakupinga ripoti ya daktari wa mifugo ambayo ilionyesha kuwa ng’ombe huyo alikuwa ameingiliwa na binadamu.
“Mahakama hii imeshindwa kung’amua kwa nini mshtakiwa angefanya kitendo kama hicho bila kujali ni kileo kipi alikuwa amebugia,” alisema hakimu.
Akijitetea, Bw Kiruga aliomba mahakama isimpe adhabu ya miaka mingi kwani hakuwa ameoa na miaka yake imesonga sana.
“Mahakama hii imeshangazwa na jinsi mshtakiwa amejitetea akisema kuwa hajaoa na ilhali miaka imesonga sana. Jambo ambalo hakuiambia mahakama  sababu za yeye kutooa.
Labda alipanga kumuoa huyu ngo’mbe. Ama huyu ng’ombe alikuwa suluhisho mbadala?” aliuliza hakimu Wendy akitoa hukumu hiyo.
Swahili hub.

No comments: