MCHUMBA WA MTU ATUPWA SEGEREA BAADA YA KUNASWA AKIJIUZA JIJINI DSM
Kauli ya wahenga isemayo Siku
za mwizi ni 40 ilitimia Jumatatu iliyopita kufuatia msichana
Pili Baraka (21) aliyevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake hivi karibuni
kujikuta akitupwa Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kunaswa kwa tuhuma za
ukahaba,
Mrembo huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Sokoine Drive Jijini DSM na kusomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timothy Lyon.
Akisoma shitaka hilo, Magodi alisema: Agosti 5, mwaka huu, saa nane usiku, Pili alinaswa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar akifanya biashara ya ukahaba.
Aliposomewa shitaka lake hilo, Pili aliinamisha kichwa na kujibu kwa kifupi: Si kweli.
Licha ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akijitetea kabla ya kupandishwa kwenye karandinga kwenda Segerea, Pili aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma asiende kuilia Sikukuu ya Idd, Segerea kwa kuwa mchumba’ake yuko safarini kikazi na hakuwa na mtu mwingine wa kumwekea dhamana, ombi ambalo lilikataliwa.

GPL

No comments:
Post a Comment