Saturday, August 10, 2013

MCHEZO WA NGUMI WAFANA IDD MOSI MJINI MTWARA IDEFONCE MNALI WA BLACK MAMBA MTWARA AMCHAKAZA SHAHA KASIMU WA MZIMUNI DSM
Mabondia kutoka club za  black Mamba ya mtwara na  Mzimuni wa Dsm wakisubiri kukaguliwa na mgeni rami kamanda wa police mkoani mtr Linus Sinzumwa.
Burudani haikuwa nyuma Mtwara Dancers wakifanya vitu vyao
Wamuzi kamishna Kulwa Makaranga Kushoto na Riadha Kimweri katikati wakiwa na Daktari wa mchezo
Meneja wa Black Mamba Mahamudu Sinani akiwatambulisha wageni
Mgeni rasmi Kamanda wa polisi mkoani Mtwara Linusi Sinzumwa akijiandaa kusoma hotuba
t
Kamanda Sinzumwa kiwatakiwa wachezaji mchezo mwema na wa amani
Ndonga zimeanza Abdalah na Taliki 
Ashrafu na Selemani
Shongo akienda chini baada ya makonde mazito toka kwa Mwl Musa
Mwl Musa (teache alone) akifa nya vitu vyake dhidi ya Shongo




Idefonce Mnali na Shaha Kasimu

Bondia anayechipukia mkoani mtwara Idefonce Mnali kutoka katika club ya Black Mamba  jana usiku wa ameweza kumchakaza bondia Shaha Kasimu katoka katika club ya Mzimuni Mogomeni DSM katika mchezo usio na ubingwa wa uzito wa Super Middle uliopigwa katika dimba la Nangwanda sijaona mjini Mtwara sikuku ya Idd Mosi.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa round sita, Idefonce  aliweza kumchakaza Shaha kwa point 58 kwa 56.

Katika Mpambano huo ambao Mgeni rasmi alikuwa kamanda wa police Mkoani Mtwara, Linus Sinzumwa  ulitanguliwa na mapambano manne ya utangulizi.
Pambano la kwanza liliwakutanisha watoto Abdalh Ashrafu na Taliki maafudhi na Abdalah Ashraf kuibuka kidedea kwa point 30 kwa 27.
Mpambano uliofuata ulikuwa ni kati ya Ashrafu Abdalah wa Black Mamba na Seleman Shabani wa Mzimuni katika uzito wa Fly Weight Raound nne na hatimaye wababe hao kwenda sare kwa kufungana point.
Mpambano mwingine wa kuvutia wa uzito wa Light Welter Weight ulikuwa ni kati ya Muhamedi Ahamad (Penta boy) wa balack Mamba na Bahati kalembo  wa Mzimuni ambapo Bahati aliweza kumshinda Penta Boy kwa point 39 kwa 38.
Na mpambano wingine ulikuwa ni kati ya Mwalimu Musa  wa Mzimuni na Shongo Ally wa Black Mamba, ambapo Shongo alitandikwa kwa Knock Out round ya pili ambapo alikenda chini mara mbili na kushindwa kuendelea na mchezo. 

Mapambano yote yalichezeshwa na kamishna wa ngumi wa kimataifa wa IBF, TBC na AUB Kulwa Makaranga akisaidiwa na Riadha Kimweli.

No comments: