WANAUME 45 WAKAMATWA KWA KUFANYA UKAHABA KENYA
![]() |
Mshoga |
POLISI
mjini Thika wanazuiliwa wanaume 45 ambao walikamatwa usiku wa kuamkia juzi kwa
kushukiwa kuuza ngono katika katika mji wa Thika na viunga vyake.
Katika
msako mkali uliodumu masaa matatu, polisi walinasa wanaume hao wengi wao
wanafunzi wa vyuo vilivyo eneo hilo, baada ya wafanyabiashara mjini humo
kulalamika kwamba ukahaba umezidi.
OCPD wa Thika Paul Letting alisema wengi wa wanaume hao watafikishwa kortini
kujibu mashtaka ya kurandaranda wakiwa na lengo la kuuza ngono.
Alisema
maafisa wa polisi wameweka mikakati ya kufagia makahaba wote Thika ambao
alisema wameongezeka kutokana na kukamilika kwa barabara kuu ya kutoka Thika
kuelekea Nairobi.
Msemaji wa
Wauzaji Ngono eneo hilo Barrack Ondiek alithibitisha kwamba wakahaba wa kiume
wameongezeka sana mjini humo katika kipindi cha miezi sita iliyopita baadhi
wakiwa wametoka Mombasa, Mlolongo na Nairobi.
Alisema
kati ya 45 waliokamatwa, 10 ni wa kutoka Thika. Wengine ni wanafunzi wa chuo
kikuu kimoja ambao Jumanne walifikishwa kortini Thika na wakaachiliwa huru kwa
dhamana.
Alifichua
kuwa ushoga unaenea sana Thika kutokana na kusajiliwa kwa Chama cha Mashoga
mjini humo miezi mitatu iliyopita na sasa chama hicho kina wanachama zaidi ya
200.
No comments:
Post a Comment