TAARIFA KUTOKA TFF LEO
MTIHANI
WA UWAKALA WA WACHEZAJI, MECHI SEPT 26
Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kutakuwa na
jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za
kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni
mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini. Kwa ambao wangependa kufanya
mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha
nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo
watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.
Mtihani huo
utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika
90. Mpaka sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na
FIFA. Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa
na Said Tully.
WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi
wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili
(physical fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.
Mtihani huo
utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na
Morogoro.
Kituo cha
Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara,
Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Kituo cha
Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani,
Ruvuma na Tanga.
Washiriki
wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si
vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika
mtihani huo.
RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14
RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14
Ratiba ya
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo
katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini)
inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu. Kundi A linaundwa na timu za
Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi
Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa)
na Polisi (Morogoro).
African
Lyon (Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es
Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam),
Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi
B. Timu za kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba
(Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United
(Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).
Unakumbushwa
kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa hatua ya
kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili ni
Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment