AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMLAWITI NA KUMZALISHA BINTI YAKE
Yusufu Amani |
Yusufu Amani akikwepa kamera za waandishi |
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa |
MAHAKAMA
ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani humo
baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa
kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha
mashitaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakamani hiyo
Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39)
anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na
mkewe.
Alisema
kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha
makosa ya kuzini.
Akisoma
Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi
na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa
watoto wote.
Aliongeza
kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule
ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi
ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema
mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na
kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana
yoyote mtaani kwao.
Hakimu
Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa
Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa
Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema
ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa,
Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa
Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya
Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha
kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe
adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa
kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya
hukumu.
Kutokana
na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba
ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali
katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa
hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na
kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “
mfa maji haachi kutapatapa”
Na
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment