TIMU YA AL MASRY YAONDOLEWA ADHABU YA KUFUNGIWA KUTONA NA VURUGU ZA PORT SAIED
CHAMA cha Soka nchini Misri-EFA kimetangaza kuiondolea
adhabu timu ya Al Masry kwa kuiruhusu kushiriki msimu mpya wa Ligi Kuu nchini
humo ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.
Al Masry walifungiwa mwaka mmoja na EFA baada ya vurugu
zilizotokea Port Saied Februari mwaka jana ambapo mashabiki zaidi ya 72 wa Al
Ahly waliuawa uwanjani.
Msemaji wa EFA Azmy Megahed amesema Mahakama ya Usuluhishi
wa Michezo ya CAS imeiruhusu Al Masry kucheza na tayari wameshalipa ada yao ya
ushiriki katika ligi hiyo.
Hata hivyo Al Masry watakabiliwa na tatizo la kutafuta
uwanja mwingine wa kutumia katika mechi zao za nyumbani kutokana na adhabu ya
kufungiwa miaka mitatu uwanja wao wa Port Saied ikiwa bado
haijamalizika. Maofisa awa Al Masry wanataka mechi zao kuchezwa Al
Ismailiya lakini majeshi ya ulinzi walikataa wazo hilo kwasababu za kiusalama.
CAF YATUPILIA MBALI OMBI LA AL AHLY KUSOGEZA MECHI YAO DHIDI YA ORLANDO PIRATES.
SHIRIKISHO
la Soka barani Afrika-CAF limetupilia mbali maombi ya Al Ahly waliotaka
kusogeza mbele mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya Orlando
Pirates iliyotakiwa kuchezwa Agosti 4 kwa ajili ya mfungo wa Ramadhan.
Katika
taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa katika mtandao wake walithibitisha kupokea
barua kutoka CAF ya kukataliwa ombi lao hilo. Mapema Jumapili iliyopita
mkurugenzi wa michezo wa Al Ahly Sayed Abdel Hafiz aliviambia vyombo vya habari
nchini Misri kuwa klabu hiyo imeomba mchezo huo kusogezwa mbele kwa siku tano
ili kuepuka matatizo wachezaji wake waliyokutana nayo katika mchezo dhidi ya
Zamalek. Hafiz alidai kuwa wachezaji wake walikabiliwa na wakati mgumu
katika mchezo huo baada ya kukataa kufungua na kucheza mchezo huo katika
kipindi cha mchana kilichokuwa na joto kali.
Klabu hiyo
pia imetakiwa kutafuta uwanja mwingine kwa ajili ya mchezo huo wa kundi A baada
ya jeshi kuwakatalia uwanja wao wa Air Defence uliopo jijini Cairo kwasababu za
kiusalama
No comments:
Post a Comment