KENYA KULIKONI JAMANI, MWANAMUME MWINGINE ASHTAKIWA KWA KUJAMIIANA NA KONDOO.
![]() |
Mji wa Nakuru. Picha/SULEIMAN
MBATIAH
|
MWANAMUME
mwenye umri wa makamo alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru na kushtakiwa kwa
kujamiiana na kondoo.
Barnabas
Njuguna, alishtakiwa kuwa mnamo Julai 23, 2013, katika shamba la Nyaituga
lililo Mirangine, Kaunti ya Nyandarua, alijamiiana na kondoo aliyekuwa
amefungwa katika shamba hilo linalomilikiwa na Joseph Mwangi
Mahakama
iliambiwa kuwa Bw Njuguna alipatikana akiwa amevua nguo za sehemu ya chini ya
mwili akitenda kitendo hicho.
Alipokabiliwa,
alijaribu kutoroka na kumpelekea mlalamishi, Bw Mwangi, kukamata suruali yake
iliyokuwa chini ya magoti, hadi akamwangusha chini.
Mahakama
ilizidi kuambiwa kuwa Bw Mwangi alipiga kelele zilizopelekea majirani
kufululiza hadi bomani mwake na kumsaidia kumpeleka mshtakiwa hadi katika kituo
cha polisi.
Wanakijiji
walimwita daktari wa mifugo aliyemkagua kondoo huyo na kuthibitisha kuwa
mshtakiwa alijamiiana naye, kulingana na maelezo mbele ya mahakama.
Ghadhabu
zilipozidi kupanda, wanakijiji waliamua kumuua Bw Njuguna, ingawa walizuiliwa
walipokuwa karibu kufanya hivyo.
Polisi
waliowasili hapo kwa haraka walifanikiwa kumuokoa mshtakiwa huyo kutoka
mikononi mwa wanakijiji.
Alipofikishwa
mbele ya Hakimu Mkuu Samuel Mungai, Bw Njuguna aliyeonekana akiwa mwingi wa
wasiwasi alikiri mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 au
Sh100,000 taslimu, huku kesi hiyo ikipangiwa kusikizwa Septemba 9.
No comments:
Post a Comment