Tuesday, June 18, 2013

MECHI ZA CECAFA KUENDELEA KAMA KAWAIDA LICHA YA TAHARUKI
Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye

KORDOFAN, Sudan
MASHINDANO ya Cecafa Kagame Cup yataendelea kama yalivyokuwa yamepangwa kuanzia Jumanne ya leo nchini Sudan licha ya taharuki kuhusiana na hali ya usalama katika eneo la Kordofan.

Pamoja na taarifu kuwa mwanajeshi mmoja mlinda usalama wa Umoja wa Mataifa kuuawa kufuatia mlipuko wa bomu, katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye ameshikilia msimamo wake kuwa dimba hilo litaendelea kama lilivyopangwa.

Musonye amesema mechi ya ufunguzi itaandaliwa katika eneo linalokumbwa na tishio la usalama la Kordofan Kusini katika uwanja wa Kadugli kati ya El Hilal na Uganda Revenue Authority.

URA ambao ni mabingwa wa zamani wa Uganda ni miongoni mwa timu tatu ambazo zilijumuishwa kushiriki dimba hilo dakika za mwisho mwisho baada ya kujiondoka kwa klabu za Tukser FC ya Kenya na Simba na Yanga za Tanzania.

“Hakuna jambo lolote ambalo litazuia dimba hili kuendelea kama lilivyopangwa awali. Timu zote 11 ziko tayari kwa mechi hizi hasa baada ya kuwasili jijini Khartoum kati ya Jumamosi na Jumapili.

Timu hizo na maafisa wake walisafirishwa kwa ndege hadi eneo la Kadugli na El Fasher Jumapili,” alisema Musonye.

Fainali za mashindano hayo ambayo hudhaminiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame itafanyika Julai 2

No comments: