MWANAMUME AKAMATWA KWA KUSHIRIKI NGONO NA NG'OMBE
![]() |
Mfanyakazi wa Kampuni ya Kusambaza Maji Kikuyu, aliyetambuliwa kwa jina Kariuki baada ya kutiwa mbaroni Juni 12, 2013 |
MAHAKAMA ya Kikuyu nchini Kenya ilimwachilia huru mwanaume aliyesemekana kuwa
alishiriki kitendo cha ngono na ng’ombe kwa dhamana ya Sh10, 000 huku
wakingojea uchunguzi zaidi dhidi ya shtaka hilo.
Bw Justin Kariuki aliachiliwa na
polisi wa Kikuyu ambao wanaendeleza uchunguzi kuhusu madai ya wanavijiji wa
Mugumo-ini waliosema kuwa mzee huyo alikuwa amezoea tabia ya kushika ng’ombe.
Inadaiwa kufumaniwa akichafua
ng’ombe wa tatu.
Polisi wanashuku mzee huyo
anasingiziwa kwani wakazi wengi wa Mugumo-ini huiba maji ya kampuni ya Kikuyu
Water na wengine wako na deni kubwa katika kampuni hiyo ambayo Bw Kariuki
anafanyia kazi.
Mpema wiki hii mwanaume huyo alikamatwa na polisi Kikuyu, Kiambu baada ya
kudaiwa kushiriki ngono na ng’ombe mwenye mimba eneo la Kiambaa.
Mwenye ng’ombe bwana David Munene aliomba mzee huyo atozwe faini ya Sh150, 000 akisema hawezi
tena kuendelea kumfuga ng’ombe huyo au kunywa maziwa yake.
Munene
alisema kuwa ngombe huyo ana mimba ya miezi saba na alishtuka sana kupata mzee
huyo akifunga suruali yake ndefu huku akiwa na kinyesi cha ng’ombe nguoni mwake
baada ya kufanya ngono na mnyama huyo.
Aliongeza
kuwa mshukiwa alikuwa amechukua viti viwili ambavyo wao hukalia wakati
wanakamua ngombe, na kuviwekelea kimoja juu ya kingine ili afikie ngombe vizuri
na kufanya kitendo hicho cha aibu.
“Nilimpata
tu akifunga suruali yake ndefu na akajaribu kutoroka lakini tulimshika na
kujulisha polisi,” alisema Bw Munene.
Ilisemekana
kuwa Kariuki ameajiriwa katika Kampuni ya Maji ya Kikuyu na hutembea nyumbani
mwa watu akiangalia kiasi cha maji ambacho watu wametumia kazi ambayo
hujulikana kama kusoma mita.
Bi
Mary Nyambura alisema kuwa kama familia wanataka mzee huyo alipe Sh100, 000 kwa
ngombe huyo, na Sh50 ,000 kwa ajili ya ndama aliye tumboni kisha mshukiwa
achukue ngombe huyo kuwa wake.
Mkuu
wa Polisi Joshua Opiyo alithibitisha tukio hilo na kusema alitiwa nguvuni katika stesheni ya polisi ya Kikuyu, lakini
bado ngombe yumo kwenye zizi la mwenyewe,” alisema Bw Opiyo.
Alikubaliana
na familia kuwa ni jambo la kuchafua roho kunywa maziwa ya ngombe yule, lakini
akaomba wenye ngombe kusubiri uamuzi wa korti.
Ilibidi
polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya watu ambao walikuwa wamejaa mahali
ambako tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Migumo-ini wakitaka kumpiga
mzee huyo.
Mkaazi
wa Mugumo-ini, Paul Munga alisema ni mara ya tatu mzee huyo kumdhulumu ng’ombe.
“Alikuwa
ameshika ng’ombe wa mamangu lakini hakupata kifungo, aliachiliwa na kuendelea
na tabia yake,” alisema Bw Munga.
Wakazi
wana hofu kuwa Kariuki ataachiliwa tena, lakini wamesema, “Kariuki asifike
kijiji cha Migumo-ini tena kwani anatuharibia ngombe zetu.”
Wakazi
wengine hata walisema atolewe sehemu zake za siri kama funzo kwa wengine na
kukomesha tabia zake mbaya
No comments:
Post a Comment