Monday, May 27, 2013



Akiwa kazini


Akitimua mbio baada kukurupushwa siku za nyuma

Akiwa amedakwa na wananchi wenye hasira leo
Kichapo kinaanza


Akishushiwa kipigo kitakatifu

AMA Kweli  mwisho  wa  utapeli ni aibu  kubwa na   wahenga walinena   kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni  kwa  wakazi  wa Miyomboni mjini Iringa wamepata  kushuhudia  kituko cha mwaka  baada ya watu  waliochoka  kuvumilia vitendo vya  kitapeli  vinavyofanywa mzee  mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.

Tapeli  huyo  mbali ya  kuumbuliwa kwa  kutakiwa  kuonyesha miguu  yake  yote  pamoja na mikono  yake  yote  bado amepata  kuchezea  kichapo  kiasi cha  kunusurika  kuuwawa na wananchi  hao wenye hasira  kali.

Kutokana na kufichuliwa kwa  siri  hiyo ya  kujiigiza  kuwa ni  omba omba mlemavu wananchi wamekuwa  wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na  kumtimua  mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua  kumkimbiza  kutoka eneo la Hazina  Ndogo  hadi miyomboni na kuanza  kumpa  kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo  vyote kuwa  si mlemavu


Tapeli  huyo mbali ya  kujifanya ni mlemavu  wa  viungo  wakati mwingine huwa anajifanya  ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama  mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu  mmoja na  kuwaomba  watu fedha za matibabu .


Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)


Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  kutokana na  kichapo alichokipata  na kuumizwa  vibaya usoni .


Hata  hivyo  inasemekana  mzee  huyo  amekuwa akiadhibiwa katika maeneo mbali  mbali kutokana na mbinu yake ya  kufuru anayoifanya  kuwa ni mlemavu  wakati si mlemavu na  kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya  kiuchumi kuliko  kuwaigiza  walemavu na  kuwa iwapo atarudia na  kukutwa akifanya  hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema  wananchi hao.



Aidha  anadaiwa chanzo cha  kichapo  cha  leo kwa mzee  huyo tapeli ni mmoja kati ya  mpenzi  wake ambae  alikuwa amemsusa na  kuhamia kwa mpenzi mwingine  kuueleza umma kuwa  huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi  wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea  wananchi kufanya udadisi .


Kabla kufukuzwa na kuchezea  kichapo tapeli huyo alifukuzwa  eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya  vijana  wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona  viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.


Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.



No comments: