MWANAMKE APELEKWA JELA MIAKA SITA KWA KUTELEKEZA WATOTO NA KUENDEKEZA UKAHABA HUKO NCHINI KENYA
![]() |
Barabara ya Koinange mjini Nyahururu.
|
Mwanamke mmoja aliyeachiliwa hivi
majuzi kutoka korokoroni baada ya miaka mitatu sasa atarejea humo kutumikia
kifungo cha miaka sita kwa kuwafungia watoto chumbani na kwenda mitaani kufanya
ukahaba.
Hakimu Mkaazi wa Nyahururu Peter Muholi alisema ni jambo la kuhuzunisha kuona
Lilian Wanjiku aliyesukumwa gerezani
kwa kosa lile lile awali, akitenda kosa lile lile na kuwafungia watoto wake
wachanga na kuzura zurura mitaani kutafuta wanaume wampe hela za kununulia
mvinyo huku akisahau ana majukumu mengine.
Kati ya Aprili 22 na 27, mshtakiwa aliwafungia watoto wake chumbani na kuwaudhi majirani wake ambao walishangaa kusikia watoto wakilia usiku kucha na kisha kuendelea kulia mchana. Waliamua kuvunja nyumba hiyo na kuwaokoa watoto hao ambao hali yao ilikuwa hafifu sana.
Hatimaye baada ya wiki nzima mama yao alifika nyumbani akiwa mlevi chakari asijue kilichokuwa kikiendelea na hakujali kujua walikokuwa watoto na baada ya kuingia na kutoka chumbani, alielekea kwa mama pima huku akijidai 'ameshinda jela wanakijiji watampeleka wapi.’
Tabia hii iliendelea kwa wiki nzima hadi majirani wakaamua kupiga ripoti kuhusu ujeuri wa mama huyo ambaye alikuwa ameachiliwa kutoka jela mnamo Februari kufuatia msamaha na idhini ya Rais ili arejee nyumbani kuwatumikia watoto wake.
Lakini, akasema Afisa wa Kurekebisha Tabia, mshtakiwa aliendelea na tabia yake ya zamani kama kawaida na hivyo ikadhihirika wazi kuwa msamaha hukumsaidia kamwe.
Bi Kimani alisema kifungo cha nje hakikumsaidia mshtakiwa kurekebisha tabia na hivyo akaomba asukumwe ndani kwa muda mrefu zaidi na watoto kupelekwa katika nyumba za watoto mayatima kwani mama yao hajiwezi.
Wanjiku alifungwa miaka mitatu kwa kutesa kila mtoto na vifungo hivyo vitaambatana.
Mshtakiwa anajiunga na kina mama wengine waliofungwa jela kwa kukaidi amri ya kutunza watoto na badala yake kujiunga na ukahaba na unywaji mvinyo kupindukia

SwahiliHub, KENYA.
No comments:
Post a Comment