Sunday, May 26, 2013

 BUYERN MUNICH YATWAA NDOO  LIGI YA MABINGWA ULAYA ROBEN AWA SHUJAA KWA BAO LA DK YA 89


WINGA Arjen Robben jana alibuka shujaa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuifungia bao la ushindi Bayern Munich katika fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Wembley, London, England ikishinda 2-1 na kutwaa Kombe hilo.

Bayern sasa wanakuwa mabingwa wapya wa Ulaya, wakirithi taji lililoachwa wazi na Chelsea kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Wajerumani wenzao, Borussia Dortmund katika mchezo mkali na wa kusisimua.

Mholanzi huyo alifunga bao hilo tamu dakika ya 89, baada ya awali kipindi cha kwanza kukosa mabao mawili ya wazi. Lakini ndiye aliyetoa pasi ya bao la kwanza kwa Bayern lililofungwa na Mario Mandzukic dakika ya 60.
Dortmund ilisawazisha kwa penalti baada ya Dante kumuangusha kwenye eneo la hatari Marco Reus na Ilkay Gundogan akaenda kufunga dakika ya 67.

No comments: