Thursday, April 18, 2013

UKISTAAJABU YA MUSA UTASHANGAA YA FILAUNI, WAZAZI SASA WAAMUA KUWABAKA WATOTO WAO WA KUWAZAA 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, imemuhukumu Abisai Joseph (40) mkazi wa Mtaa wa Kigamboni, Kata ya Shanwe mjini hapa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka sita.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya  hiyo, Chiganga Tengwa ambapo Joseph anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 18 mwaka jana, saa tano usiku akiwa nyumbani  kwake.
Awali, Mwendesha Mashtaka Ally Mbwijo, aliieleza mahakama kuwa siku hiyo ya tukio Joseph alimbaka mwanaye baada ya kumvizia wakati  alipo toka  kujisaidia haja ndogo.
Alidai kuwa baada ya kumkuta nje, alimvua nguo kisha alimweka sehemu ya mapaja yake na kuanza  kumfanyia kitendo hicho, na kwamba pamoja na mtoto huyo kupiga  kelele za kuomba msaada, mama yake aliyekuwa amelala ndani hakuweza kusikia.
Mbwijo aliongeza kuwa baada ya kumaliza kufanyiwa kitendo hicho, mtoto huyo  aliingia ndani akilia, hali iliyomfanya mama yake amuulize, lakini baba yake alijibu upesi kuwa alimkuta nje akibakwa na balozi wao wa nyumba kumi.
Alidai kuwa baada ya maelezo hayo, mama wa mtoto, Sauda Rajabu alikwenda kwa majirani kuwapa taarifa ya kitendo hicho, lakini walimshauri ende kutoa taarifa polisi.
“Akiwa hapo polisi mtoto huyo alikana kubakwa na balozi wao, bali alisema aliyembaka ni baba yake mzazi,” alidai.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne akiwemo mtoto mwenyewe aliyebakwa na mshtakiwa hakuwa na shahidi yeyote.

Hakimu Chiganga katika hukumu hiyo alisema mahakama imeridhika na ushahidi  uliotolewa na kwamba imemtia hatiani mshtakiwa kwa kuvunja sheria namba 130 (1) (e) na 131 (3) kifungu cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2009.
Alisema kutokana na kosa hilo mahakama inamuhukumu Joseph kifungo cha maisha jela ili liwe funzo kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Asajile Mwamtima (46) mkazi wa Kijiji cha Syukula, Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma za kumuingilia kimwili mtoto wake wa miaka 13 (jina linahifadhiwa) mwenye ugonjwa wa kifafa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Barakael Masaki alisema mtuhumiwa  alimuingila kimwili mtoto huyo ambaye inadaiwa aliacha shule akiwa darasa la tano mwaka 2011 kutokana na ugonjwa huo.
Alisema kuwa mtuhumiwa alimvizia mtoto huyo akiwa jikoni anapika chakula na kisha kumuingilia wakati mama mzazi, Tumikigwe Samalinga akiwa katika Kijiji cha Kiwira kumuuguza mgonjwa.
Masaki alisema taratibu za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinafanyika.
 Tanzaia daima

No comments: