Thursday, April 18, 2013


AMA KWELI NDOA NDOANO,
MKE AMSHUSHIA KIPIGO MUMEWE BAR BAADA YA KUTOONEKANA  NYUMBANI
Mume na mke wakionyeshana ubavu
Huyu ndiye mwanamke aliyeshusha sekeseke kwa mumewe akilia
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.
Habari kutoka  eneo la tukio hilo zinasema  kuwa, awali mwanamke huyo alifika katika katika eneo hilo asubuhi na mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na bwana wake huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana alikuja kishari na hata alivyokuwa akiongea na yule bwana wake tulibashiri kutokea kwa ugomvi.
 “Kweli haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai chanzo hicho.
Ikaelezwa kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo hilo.  
Global publisher.

No comments: