BI KIDUDE HATUNAYE TENA DUNIANI
![]() |
| Bi - Kidude |
Mwanamuziki mkongwe wa Muziki wa Mwambao nchini na barani
Afrika Fatuma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki
mchana huu akiwa na umri zaidi ya miaka 90.
Taarifa zinadai kuwa Bi Kidude amefariki majira ya saa 7 mchana wa leo nyumbani kwa ndugu yake huku Bububu Kisiwani Zanzibar.
Aidha taarifa hizo zinaelezo kuwa Mipango yua
kuusafirisha mwili wa Marehemu inafanyika kutoka huko Bububu hadi Nyumbani
kwake Raha Leo.
Bi Kidude alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa na
kulazwa mara kadhaa lakini kifo chake kinaelezwa pia kuchangiwa zaidi na umri mkubwa.
Msiba huu ni mzito kuwahi kutokea kwa tasnia ya
muziki na Sanaa kwa ujumla kufuatia Mchango mkubwa wa Marehemu katika kukuza
muziki halisia wa mwambao.
Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Bi Kidude Nishani ya Uhuru wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi cha uhai wake.
Nasi tunaungana na watanzania wote na wapenzi wa burudani ulimwenguni kwa msiba huu mzito.
Bi Kidude alizaliwa maeneo ya Mferejimaringo Zanzibar. Alianza muziki mwaka 1920 akiwa na miaka 13. Ni miongoni mwa wasanii wakongwe hapa nchini
wenye historia ya kipekee. Licha ya kuwa na historia ya kipekee, msanii
huyo mkongwe amejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kupitia
kazi yake ya sanaa.
Bikidude anaminika kwamba ndie msanii mkongwe kuliko msanii mwingine yoyote wa kike hapa nchini.
Msanii
huyo ni muimbaji mwenye historia ya kipekee hapa nchini na kutokana na
umahiri wake wa uimbaji na amefanikiwa kutembea nchi mbalimbali za
Afrika, Ulaya na Asia kwa ajili ya kufanya kazi zake za muziki na
kuitangaza taifa kwenye jumuia za kimataifa.
Katika
siku za hivi karibuni, mkongwe huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi
lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri ingawa hajaanza kufanya
shughuli zake za muziki.
Msanii huyo mwishoni
mwa mwaka jana, serikali ilimtunukia nishani ya heshima kutokana na
mchango wake mkubwa kwa taifa. Nishani hiyo alitunukiwa na Rais Jakaya
Kikwete, Ikulu mjini Dar es Salaam.
Rais
Kikwete alimtunuku Bikidude na wasanii wengine nishani ya sanaa na
michezo ambayo hutolewa kwa wasanii na wanamichezo mashuhuri, ambao kazi
zao za sanaa au michezo zimeipatia sifa kubwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Anaangaliwa kama malkia wa muziki wa taarab na unyago
hapa nchini ambaye kipaji chake kiligunduliwa na kuimarishwa na mkongwe
wa muziki wa aina hiyo Siti binti Saad kati ya miaka ya 1880 mpaka
1950.
Mpaka sasa
haijafahamika tarehe ya kuzaliwa ya bibi huyo kwasababu sehemu kubwa ya
historia zinazo husu historia ya maisha yake hazioani na hivyo kuwepo
na taarifa ambazo ni za kubuni.
Mwaka
2005, Bikidude alipewa tuzo ya heshima ya dunia WOMEX tuzo ambazo
zilibuniwa mwaka 1999 na mbazo wanazawadiwa watu ambao wamepata
mafanikio makubwa katika muziki au wametoa mchango mkubwa katika muziki,
umuhimu wa mtu katika jamii na hata, mafanikio ya kibiashara na kwa
upande wake ilitokana na mchango wake katika muziki na utamaduni wa
Zanzibar.
Akiwa
mdogo, Bikidude alisifiwa sana kutokana na sauti yake na katika miaka ya
1920 alianza kuimba na vikundi mbalimbali vya kiutamaduni.
Alipokuwa na umri wa miaka 13, baada ya kulazimishwa kuolewa aliamua kutoroaka na kuelekea Tanzania Bara.
Bikidude
ni moja ya waimbaji wakongwe waliozunguka nchi zote za Afrika Mashariki
akiimba taarab ambapo alitembelea miji mikubwa ya ukanda wa pwani pamoja
na bara upande wa ziwa Victoria na Tanganyika.
Mwaka 1930, alirejea Dar es Salaam na kujiunga na kikundi cha Egyptian Taarab ambacho alidumu nacho kwa miaka mingi.
Katika miaka ya 1940 alirejea Zanzibar na kujenga nyumba yake iliyokuwa ya matope na kuanza maisha mapya hapo.
Alikuwa
maarufu sana kwa shughuli za unyago ambazo ziliwaandaa masichana wadogo
kuelekea katika ubalehe na kuingia katika maisha ya utu uzima.
Ni
mtaalamu wa mambo hayo ya mila kongwe akifanya hivyo kwa wasichana
akitumia mafunzo ya kitamaduni kuwaelekeza wasichana namna ya kuishi na
waume zao na kuepuka migongano ya kifamilia na unyanyasaji wa mapenzi.
Sifa na
jina la Bikidude lilikuwa na kusifika katika jamii yote ya Zanzibari na
kuwa kielelezo cha utalii wa visiwa hivyo vya karafuu ambapo hoteli
mbalimbali kubwa na zenye hadhi ya juu visiwani humo zimekuwa zikizipa
majina migahawa ya hoteli jina la Bikidude, mfano 236 Hurumzi inatumia
jina la mgahawa wake jina la 'Kidude'.
Moja ya
nyimbo zake ambazo zilitamba na kumpatia umaarufu mkubwa mkongwe huyo ni
Muhogo wa Jang'ombe ambao ulikamata kwenye mwambao wa Afrika Mashariki.
Bikidude ni hazina kubwa na mwalimu mzuri kwani inasemekana wasanii wengi wamepata mafunzo kutoka kwake.
Pamoja na
umahiri wa msanii huyo lakini hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote hadi
sasa hivyo amekuwa na historia ya kipekee tofauti na wasanii wa sasa.
Bikidude,
amedumu kwenye fani ya uimbaji kwa zaidi ya nusu karne na kwa sasa ni
msanii pekee wa taarab mwenye sifa zilizotukuka kutokana na ukongwe wake
na umahiri wake katika kuimba taarab.

No comments:
Post a Comment