REAL MADRID KAMA BARCELONA NAYO YAKUNG’UTWA 4-1 NA BORUSSIA DORTMUND.
![]() |
Muuaji wa Real Madrid Robert Lewandowski |
MABAO manne ya Robert Lewandowski
usiku wa kuamkia leo yameipa Borussia Dortmund ushindi wa 4-1 dhidi ya Real
Madrid katika Nusu Fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.
Mabao hayo ya mshambuliaji huyo wa
Poland yanawafanya Dortmund watengeneze mazingira ya fainali ya klabu za
Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern
Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza
dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini mshambuliaji huyo akarudi na
makali zaidi kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na
67 kwa penalti.
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho
aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo hicho, sasa anatakiwa kutengeneza
mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku
Dortmund.
No comments:
Post a Comment