Mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo
(Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5
mwaka huu kwenye uwanja huo huo. Mabadiliko hayo yametokana na Serikali
kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa
zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi
washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla.
Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo. Ligi hiyo
inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam
itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka
huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi
Morogoro.
No comments:
Post a Comment