PSG NA JUVENTUS ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA
![]() |
| Juventus |
![]() |
| PSG |
KLABU
ya Paris Saint-Germain-PSG imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya
michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kusubiria kwa miaka 18 wakati Juventus
ambayo wamewahi kuchukua kombe hili mara mbili nao wametinga hatua hiyo baada
ya miaka saba kupita. PSG ambao walicheza bila kiungo nyota waliomsajili
hivi karibuni David Beckham walifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Valencia ya
Hispania katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Parc des Princes na
kupelekea kusonga mbele lwa jumla ya mabao 3-2. Huko jijini Turin.
Juventus
ambao wamewahi kuwa mabingwa wa michuano hiyo mwaka 1985 na 1996 wametinga
katika hatua hiyo baada ya kuigaragaza Celtic ya Scotland kwa mabao 2-0 na
kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 katika michezo miwili
waliyocheza. Mabao yaliyofungwa na Alessandro Matri katika kipindi cha
kwanza na Fabio Quaglirella alilofunga katika kipindi cha pili yalitosha
kuihakikishia nafasi Juventus ambao wanaongoza Ligi Kuu nchini Italia.


No comments:
Post a Comment